Financial Times (FT) ni gazeti la biashara la kimataifa kutoka nchini Uingereza. Ni gazeti ambalo hutolewa kila siku asubuhi na huchapishwa katika sehemu 24 huko London.[1] Gazeti hili, ni mshindani mkubwa kabisa wa gazeti lenye makao yake makuu huko New York City-Wall Street Journal. Hivi sasa, mhariri wake ni Lionel Barber.